Siku ya Ijumaa, shirika la intelijensia ya ndani la Ujerumani, BfV, liliitangaza AfD inayopinga uhamiaji kama shirika lenye "msimamo mkali", kwa kuashiria kauli mbalimbali za viongozi waandamizi wa chama hicho za "chuki dhidi ya wageni, chuki dhidi ya jamii za walio wachache, na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu". Kuhusishwa na vitendo hivyo kunaiwezesha Polisi kufuatilia kwa karibu shughuli za chama hicho.
Kufuatia hatua hiyo, makamu wa rais wa Marekani ametoa mjibizo kupitia ujumbe alioweka kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema: "Chama cha AfD ndicho chama maarufu zaidi nchini Ujerumani, na kinawakilisha zaidi Ujerumani Mashariki. Sasa watendaji wa serikali wanajaribu kukiangamiza".
"Magharibi kwa pamoja iliubomoa Ukuta wa Berlin. Na sasa umejengwa upya - na si na Wasovieti au Warusi - , bali na serikali ya Ujerumani", ameongezea kueleza Vance.
Kiongozi mwenza wa chama hicho cha mrengo wa kulia nchini Ujerumani, Alice Weidel, ameituhumu serikali kuwa inajaribu kuzima upinzani.
Katika ujumbe alioweka kwenye mtandao wa X, Weidel amesema: "kwa vile AfD ndicho chama chenye nguvu zaidi katika uchaguzi sasa, wanataka kukandamiza upinzani na uhuru wa kujieleza" .
AfD ilianzishwa mwaka 2013 na ilishka nafasi ya pili katika uchaguzi wa shirikisho uliofanyika mwezi Februari kwa kunyakua viti 152 katika bunge la Ujerumani Bundestag lenye viti 630.../
342/
Your Comment